Aliyekuwa Waziri wa masuala ya kigeni Marekani Colin Powell ambaye alikuwa mmarekani mweusi wa kwanza kuwa Waziri wa masuala ya kigeni amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 kutokana na matatizo ya Uviko 19.

Aidha Waziri Colin alikuwa afisa mkuu wa jeshi ambaye alipanda hadhi hadi kuwa Mmarekani wa kwanza mweusi kuwa Waziri wa masuala ya kigeni mwaka 2001 chini ya uongozi wa Rais George W Bush.

Hata hivyo taarifa inasema kuwa Colin alikuwa amepata chanjo kamili dhidi ya ugonjwa huo kabla kifo chake.

Colin alikuwa mshauri wa kijeshi kwa viongozi wengi wa kisiasa, alihudumu na kujeruhiwa nchini Vietnam, uzoefu ambao baadaye ulimsaidia kuandaa mipango yake ya kijeshi na kisiasa.

Machinga Dar waongezewa siku 12
Rais Samia asisitiza nidhamu