Mmilikiwa wa klabu ya Paok Salonika inayoshiriki ligi kuu nchini Ugiriki, Ivan Savvidis alilazimika kuingia ndani ya uwanja huku akiwa amebeba bastora kiunoni kufuatia bao la timu yake kukataliwa wakati Paok ikicheza na AEK Athens kwenye mchezo wa ligi hiyo.

Mshambuliaji wa Paok, Fernando Varela alifunga bao dakika za mwisho kwenye mchezo huo na kukubaliwa na mwamuzi wa katikati lakini mwamuzi wa pembeni alikataa kwa kuonesha mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Kutokana na tukio hili mmiliki wa klabu hiyo ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini humo alishuka kutoka jukwaani na kuiingia uwanjani akiwa ameongozana na walinzi wake huku akionekana amebeba bastora kitendo kilichozua taharuki miongoni wa mashabiki na waamuzi wa mchezo huo.

Maofisa wa timu ya AEK Anthers wamesema mmiliki huyo alikuwa akimtishia mwamuzi kabla ya kutolewa uwanjani.

Mchezo huo ulihairishwa kutokana na tukio hilo baada ya vurugu za hapa na pale kuzuka.

Paok ambayo ipo katika nafasi ya tatu na pointi zake 50 katika msimamo wa ligi kuu nchini humo, ilikuwa ikihitaji ushindi ili iweze kuisogelea timu ya AEK Anthers inayo kamata nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 55, ikifuatiwa na Olympiacos yenye pointi 53.

 

Mke wa Rais kuongoza mkutano kuhamasisha amani Nigeria
Nigeria kutoa tiba ya bure kwa wananchi wake

Comments

comments