Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg ametoa utetezi wake dhidi ya tuhuma zilizoibuliwa kuwa mtandao huo ulisaidia kueneza habari za uongo zilizompandisha kisiasa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump.

Akihutubia hivi karibuni katika mkutano wa kiteknolojia uliofanyika California nchini Marekani, Zuckerberg alisema kuwa Facebook haipaswi kuwajibishwa kwa kilichotokea.

“Mtazamo kuwa Facebook ilifanya ushawishi katika uchaguzi uliopita kwa namna yoyote ni mawazo ya ukichaa,” alisema Zuckerberg.

“Na kama unaamini katika hilo, sidhani kama uliutia akilini ujumbe wa wanaomuunga mkono Trump wanachojaribu kusema katika uchaguzi huu,” aliongeza.

Tafiti zimeonesha kuwa habari za kugushi kuhusu Trump zilisambazwa sana kupitia Facebook kuliko habari zilikuwa na mantiki, hali inayodaiwa kumpa umaarufu bilionea huyo aliyeshinda uchaguzi na kuishangaza dunia.

Majaliwa aongoza Wabunge kuaga mwili wa mbunge Hafidh Ally
Video: 'Kama Trump amefanikiwa, basi nchi inafanikiwa' - Obama