Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Melo ambaye ni mmoja wa waasisi wa mtandao huo amesomewa mashtaka matatu katika kesi tatu zinazomkabili, ikiwa ni shtaka moja kutoka katika kila kesi.

Kati ya mashataka hayo, moja ni kuendesha shughuli za mitandao ya kijamii bila kusajiliwa na mengine ni kuzuia upelelezi wa polisi.

Bosi huyo wa Jamii Forums alikwama kupata dhamana baada ya kushindwa kukamilisha sharti la kuwa na wadhamini wawili, akiwa na shahidi mmoja pekee. Hivyo alirejeshwa rumande hadi kesi hiyo itakaposilikizwa tena.

 

Mfanyakazi ajirusha kutoka ghorofa ya saba Dar
Afande Sele aanika sababu za kuitosa ACT Wazalendo