Nchini Kenya, Mmiliki wa shule katika eneo la Karatina, kaunti ya Nyeri amekamatwa kwa kukiuka agizo la rais Uhuru Kenyatta akizitaka shule zote nchini humo kufungwa kufuatia tishio la virusi vya corona.

Martha Wangai, mmiliki wa shule ya msingi Beracha Academy alitiwa mbaroni na kuhojiwa na kamati ya maafisa wa usalama baada ya shule hiyo kuendelea na shughuli za kawaida za masomo.

Kufuatia tangazo la Rais, taasisi zote za kielimu nchini zimetakiwa kufungwa katika hali ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

Afisa mkuu wa Elimu wa shule hiyo neo, Lucy Mbae amesema kuwa wanafunzi 19 wa darasa la nane walikuwa darasani wakati polisi walipovamia shule hiyo leo ya Jumatano, Machi 18, 2020.

Mbae alifichua kwamba mwalimu mkuu alitoroka na kuwaacha watoto peke yao na ndipo wanafunzi hao akawaelekeza wakae katika boma la mmiliki wa shule hiyo.

Aidha, Rais Uhuru Kenyatta wakati akitangaza hatua zilizochukuliwa na serikali kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona itakumbukwa kwamba mnamo Jumapili, Rais Uhuru Kenyatta alitoa agizo kwamba taasisi zote za elimu zifungwe kuanzia Jumatatu kwa shule za kutwa na zile za mabweni kufikia Jumatano.

Vyuo vikuu vinatarajiwa kufungwa kufikia Ijumaa.

Rukwa: wahukumiwa kwa kuoa wahamiaji haramu
Video: Ni haramu mgonjwa wa Corona kuingia Msikitini - Mufti