Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na roli la mizigo katika eneo la Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilihusisha basi la Safari Njema lililokuwa safarini kutoka Dodoma likiingia Dar es Salaam na roli lilikuwa na mzigo wa saruji.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda alithibitisha madhara ya ajali hiyo na kueleza kuwa majeruhi hao 10 walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

“Chanzo cha ajili bado tunakifuatilia lakini magari yote yaliteketea kwa moto,” alisema Kamanda Kaganda na kuongeza kuwa abiria wengi walikuwa salama.

Alisema baada ya ajali hiyo, baadhi ya vijana wasio waaminifu walianza kuiba saruji katika roli hilo lakini Jeshi la Polisi liliwadhibiti.

Diwani apost picha zake za utupu kwenye grupu la Whatsapp la Bunge
Polisi azua kizaazaa baada ya kumpigia saluti Profesa Lipumba