Makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amekanusha madai kuwa anapanga njama ya kupindua serikali ya Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Waingereza mnamo mwaka wa 1980.

Akizungumzia madai hayo kwa mara ya kwanza tangu yaibuke mwaka moja uliyopita, Mnangagwa ambaye amekuwa akihudumu kwenye serikali tangu Zimbabwe ilipopata uhuru, amesema kuwa ataendelea kusimama na Rais Mugabe.

“Kwa mara nyingine nawahakikishia kuwa nitaendelea kusimama na Rais Mugabe ambaye amefanya mengi kukomboa nchi hii,” alisema. “Sijaenda kinyume na msimamo huu, aidha kwa mawazo au vitendo kwa wakati wowote,” – Emmerson Mnangagwa

Mnangagwa amesema hayo kufuatia taarifa ya Taarifa ya Rais Mugabe akimtaka akanushe madai hayo mbele ya umma ili kudhibitisha kuwa si ya ukweli.

Mohamed Dewji "Mo" Awashukuru Wanachama Wa Simba
Rooney: Sina Muda Zaidi Kwenye Timu Ya Taifa