Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema kuwa mwanasiasa wa upinzani, Tendai Biti ameachiliwa huru na mahakama baada ya yeye kuingilia kati.

Ameyasema hayo kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambapo ameandika kuwa anataka kuwepo kwa hali ya amani nchini humo, lakini amesisitiza kuwa ni lazima taratibu za kisheria zifuate mkondo wake.

Aidha, Tendai Biti alikamatwa kwa tuhuma za kuutangazia umma wa Zimbabwe kuwa chama cha upinzani MDC kimeshinda uchaguzi wa hivi karibuni, kitendo ambacho kinatajwa kuwa kilichochea vurugu kwa wananchi.

Hata hivyo, Mwanasiasa huyo alikamatwa alipokuwa akijaribu kutorokea Zambia na kurudishwa nchini Zimbabwe, ambako anakabiliwa na tuhuma za uchochezi.

 

Video: Tuna mtihani mzito sana, amekufa Kanumba sasa Majuto - Flora Majuto
Philippe Coutinho atuliza kiu yake FC Barcelona