Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametaka wanachama wa Chama cha Zanu-PF kuachana na nyimbo za kumsifu na kuwataka watilie mkazo wimbo wa Taifa na nyingine zinazozungumzia ukombozi.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa chama hicho ambapo amewataka kutambua kuwa yeye ni Rais wa watu wote na wala si wa kikundi fulani.

Aidha, Mkutano huo ulikuwa wa kumuidhinisha Mnangagwa kuwa Mkuu Mpya wa chama na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018. na kumvua rasmi uongozi aliyekuwa kiongozi mkongwe wa chama na Serikali ya Zimbabwe, Robert Mugabe,

“Huu si wakati wa kutambiana kuwa kundi gani limeshinda bali kila mwanachama anapaswa kuzingatia mahitaji ya wananchi ambao wanataka maendeleo,”amesema Mnangangwa

Hata hivyo, Rais huyo amesema wanachama wanapaswa kurekebisha uchumi ikiwa wanataka wawe na nafasi ya kushinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

Palestina yashikili msimamo wake kuhusu Jerusalem
ANC wakutana kumchagua mrithi wa Zuma