Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti ameagiza wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite (WanaApolo) wapite bila kulipa kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini hayo hadi hapo utaratibu wa kulipia sh70,000 ili wapatiwe vitambulisho vya kupita utakapofanyika.
 
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa madini mkoani humo , ambapo amesema kuwa wanaApolo watapita bila kulipa chochote kwenye lango hilo hadi hapo vitambulisho maalum vitakapoandaliwa ambavyo watalipia kila mmoja sh. 70,000 kwa mwaka mmoja.
 
Amesema kuwa wamekubaliana kwenye kikao cha wamiliki wa migodi na wanaApolo kuwa suala la malipo ya mishahara au asilimia 10 pindi madini yakitoka wataamua wao wenyewe.
 
“Baada ya serikali kukubaliana na pendekezo lenu la kuachana na suala la mishahara ambalo lipo kisheria inabidi ikusanye kodi ya mshahara na tozo ya uendelezaji ufundi stadi,” amesema RC Mnyeti.
 
Naye Mbunge wa jimbo la Simanjiro, James Ole Millya amesema kuwa wanamshukuru Mnyeti kwa uamuzi huo kwani utawanufaisha watu wengi, ambapo amewataka wamiliki wa migodi na wachimbaji wote kutimiza wajibu wao huku wakitilia mkazo suala la ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo.
 
  • Prof. Lipumba atangaza maombi
 
  • Aliyeikataa kesi ya Zitto kuhusu CAG asifiwa na CJ
 
  • Zengwe laibuka mgao wa fedha za Tasaf
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, (Marema) Justin Nyari alisema Mnyeti ameweka historia kwa tamko hilo kwani baadhi ya wachimbaji waliondoka ila sasa watarudi.

Video: Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM, UDSM yapongeza hatua zinazofanywa na JPM
Ni lazima mnieleze ni kwanini hamjamaliza kugawa vitambulisho?- JPM