Serikali imesema inaandaa mwongozo kwa Wakuu wa Mkoa, Paul Makonda na Alexander Mnyeti baada ya kutoa matamko ya kusimamisha na kuvunja shughuli za mabaraza ya kata.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu mkuu Ofisi ya Rais, Mussa Iyombe ambaye amesema.

” Tunakamilisha mwongozo kuhusu suala hilo wiki hii, fanyeni subira” amesema Iyombe.

Mwongozo huo ni kufuatia hatua za kisheria zilizochukuliwa na wakuu hao wa  Mkoa bila kufuata taratibu na kanuni, ambapo wakuu hao waliwasimamisha kazi mabaraza ya kata kushughulikia maswala yote ya ardhi ambapo kikatiba uamuzi huo unaweza kutolewa na Wizara inayohusika na masuala ya ardhi.

Iyombe amesema tayari wamemalizana na Makonda baada ya kutoa ufafanuzi kwa njia ya maandishi akidai kuwa hakusimamisha mabaraza hayo kufanya kazi.

” tulimtaka  atuandikie barua ya kutueleza na tayari ameshafanya hivyo, tumemalizana naye kwa maandishi, hakusimamisha mabaraza hayo kufanya kazi” amesema Iyombe.

Aidha Mnyeti naye ametoa ufafanuzi akieleza kuwa amefanya uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kunyanyaswa , kuombwa rushwa na kunyimwa haki zao.

Ameongezea kuwa hawezi kuliacha baraza hilo liendelee kufanya kazi ilihali wananchi wanalalamika kukosa haki.

Aidha Kituo cha Sheria  na Haki za binadamu LHRC kimelaani na kukemea tabia hiyo iliyooneshwa na viongozi hao ya kuingilia muhimili wa dola.

 

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafunguliwa jalada mahakamani
Netanyahu aingia matatani, wapinzani wamtaka ajiuzulu

Comments

comments