Hatimaye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amejibu taarifa zilizosambaa hivi karibuni kuwa ameamua kukihama chama chake akipinga uamuzi wa kumpokea Edward Lowassa.

Taarifa zilizokuwa zimesambaa hivi karibuni na kuandikwa na baadhi ya magazeti nchini zilinukuu barua iliyokuwa imewekwa mtandao ikidaiwa kuwa ya Mnyika pamoja na namba yake ya simu ikieleza sababu kadhaa zilizopelekea yeye kukihama chama hicho, nyingi zikiwa zinamtaka Lowassa.

Mnyika ambaye ni mbunge wa Kibamba, amekanusha taarifa hizo kwa maneno machache alipozungumza na gazeti la Mwananchi hivi karibuni.

“Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama,” Mnyika amenukuliwa.

Hii ni mara ya tatu kumekuwa na taarifa kama hizo kuhusu Mnyika. Taarifa hizo ziliibuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 lakini zimekuwa zikiishia kuwa uzushi.

Shule ya Sekondari Lindi Yaungua Moto
Harmonize asimulia kilichomsibu baada ya kupigiwa yowe za ‘Mwizi’ Kariakoo