Viongozi wengine watatu wa Chadema waliokuwa gereza la Segerea wametoka leo machi 3,2020 baada ya kukamilisha kulipa faini ambapo viongozi waliofanikiwa kutoka ni katibu mkuu John Mnyika, Naibu katibu mkuu Salumu Mwalimuna, mbunge wa Tarime vijijini John Heche.

Mpaka sasa viongozi wote wa Chadema wametolewa isipokuwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambeye mpaka sasa hatima yake haijajulikana.

Hata hivyo siku ya jana viongozi wa chama hicho walioachiwa ni Halima Mdee(mbunge kawe), Ester Bulaya(mbunge Bunda mjini), EsterMatiko(mbunge Tarime mjini), PeterMsigwa(mbunge Iringa Mjini).

Ikumbukwe kuwa tarehe 10 machi baada ya hukumu Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kimechangisha fedha kutoka kwa wanachama wake na watu wengine ambao wameguswa na hukumu ya viongozi hao.

Magufuli: Ugonjwa huu unaua "tukidharau tutakwisha"
Corona yafika Kenya