Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ambaye ni mwanachama wa Klabu ya Simba ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha wanachama wa klabu hiyo kupitisha uamuzi wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa Simba kutoka mfumo wa sasa na kuingia mfumo wa hisa.

Muda mchache baada ya taarifa kutoka kuwa mkutano mkuu wa Simba uliofanyika jana kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, kuridhia klabu hiyo kuingia katika mfumo wa hisa kwa wajumbe 1216 waliyohudhuria mkutano huo kuunga mkono na mmoja pekee kusema hapana, MO Dewji ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe ambao unaashiria ni mtu mwenye furaha.

“Washabiki wa Simba hamjambo? Jumapili inaendaje? ?”

Mo Dewji ni mmoja wa watu wenye nia ya kuwekeza klabuni hapo kuelekea katika mchakato huo wa hisa.

Neymar Apandisha Mzuka Ufaransa
Hamad Rashid: Wanasiasa acheni kutoa kauli za kichochezi