Wapinzani wa Young Africans katika Kundi A la michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, MO Bejaia kutoka Algeria wamefanya mabadiliko katika benchi lao la ufundi.

Kocha Nacer Sandzak ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya kuchukua mikoba ya Abdelkader Amrani.

Sandzak alitarajiwa kusaini mkataba jana, (Alhamisi) kuiongoza klabu hio katika msimu ujao wa Ligi ya Algeria pamoja na kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika jitihada za kuimarisha zaidi kikosi chao, MO Bejaia wamemsajili kiungo Kamel Yesli kutoka JS Kabylie.

MO Bejaia watafungua hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa kuwakaribisha Young Africans Jumapili ya tarehe 19 katika pambano linalotarajiwa kupigwa saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Waarabu hao watawakosa wachezaji wao mlinzi wa kati Zidane Mebarakou na mshambuliaji Mouhamed Ndoye, ambao wana adhabu ya kadi.

Hizi Ndizo Rekodi Za Mbeya City FC Msimu Wa 2015-16
Chama Cha Soka Dar es salaam Chatoa Tahadhari Kwa Young Africans