Mabingwa wa soka Tanzania bara, Young Africans usiku wa kuamkia hii leo, walianza vibaya michuano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi, baada ya kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya wenyeji wao MO Bejaia.

Bao hilo pekee katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Unite Maghrebine huko Bejaia, liliwekwa nyavuni na beki Yassine Salhi katika dakika ya 20, baada ya kuzitendea haki jitihada za mshambuliaji straika Ismail Belkacemi.

Hata hivyo Young Africans walionyesha upinzani mkubwa katika dakika zote za mchezo ingawa mipango yao ya kulifikia lango la wenyeji ilikuwa ikikwamishwa na viungo wa waarabu hao huku mabeki wao wakimalizia kazi nyepesi.

Kupoteza mchezo huu si jambo zuri kwa Young Africans kutokana na hatua ya makundi jambo muhimu zaidi ni kupata pointi tatu na hii tayari ni faida kwa Bejaia walioko nafasi ya pili huku kundi likiongozwa na TP Mazembe  iliyoanza vyema michuano hiyo kwa kuitandika Medeama ya Ghana 3-1 kwenye uwanja wa Mazembe jijini  Lubumbashi.

Kundi hilo litakuwa gumu na lisilotabirika kama Young Africans wanaoshika nafasi ya tatu wataifunga Mazembe kwenye mchezo wao utakaopigwa Juni 28 katika dimba la Taifa jijini Dar na pia Bejaia ikipoteza ugenini dhidi ya Medeama.

Nape asema Lowassa ni alama ya ufisadi, ampa ushauri mgumu
Video: Watatu wamepoteza maisha baada ya kula mihogo inayosadikiwa kuwa na sumu, Morogoro