Bilionea na mfadhili wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji amewapa nguvu ya ziada wachezaji wa timu hiyo baada ya kujinyakulia ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye kiuweledi ni mkufunzi wa soka alikuwa miongoni mwa walioshuhudia mtanange huo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mo amewashukuru wachezaji, viongozi na mashabiki wa timu hiyo kwa kufanikisha ushindi huo, akisisitiza kuwa wakiendelea na mshikamano wao watafanikisha azma ya kuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

“Huu ni ushindi wetu sote! Nawapongeza na kuwashukuru wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama, mashabiki, na wapenzi wote wa SIMBA! 🙏🏽 Safari ndio kwanza inaanza. Tuendeleze mshikamano wetu ili tufikie lengo letu la kuwa mabingwa wa Afrika, Insha’Allah #NguvuMoja,” ametweet.

Simba ambao wanatumia kauli mbio ya ‘Yes We Can’ (Ndio Tunaweza) walifanikisha ushindi huo jana kupitia kwa wachezaji wake Emmanuel Okwi na Meddie Kagere.

Kagere alipachika magoli mawili katika dakika ya 51 na dakika ya 67 ya mchezo, akiongezea idadi kwenye goli la awali la Okwi lililopachikwa kimiani katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

 

View this post on Instagram

 

Yes We Can Done it

A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on


Kwa matokeo hayo ya jana, Simba inaongoza katika kundi lake katika hatua ya makundi, hali inayowapa nguvu zaidi za kuweza kupenya katika hatua hiyo.

Shein awakingia kifua JPM, JK kutohudhuria miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 13, 2019

Comments

comments