Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Mohammed Dewji amesema suala la usajili wa kikosi cha klabu hiyo kwa msimu ujao wa 2021/22, litaendelea kufanywa siri.

Mo amesema hilo alipozungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa (Julai 30) jijini Dar es salaam, huku akiwataka radhi Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kwa maamuzi ya kufanya siri suala la usajili.

Mo Dewji amesema klabu ya Simba inashindana na timu kubwa Afrika kusajili, hivyo wanalazimika kufanya usajili wao kuwa siri hadi watakapokamilisha.

“Tukishawapata hao wachezaji tutaeaeleza mashabiki wetu, tunawaomba radhi kwenye hilo,” amesema Dewji.

Simba SC itafanya usajili wa wachezaji watakaoboresha kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika, huku ikitarajia kuwaacha baadhi ya wachezaji wake na wengine kuwatoa kwa mkopo.

Bilioni 8.59 kumaliza tatizo la umeme Kilimanjaro
Tusker FC yavuruga ratiba Kagame Cup 2021