Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’ atazungumza na waandishi wa habari ndani ya majuma mawili yajayo.

Dewji amethibitisha mpango huo, huku wingu zito likiwa limetanda Msimbazi, kufuati kitendawili kati ya Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez na Mkuu wa Idara ya Habari Haji Manara.

‘Mo’ amesema katika mkutano huo ataweka wazi mambo yote kuhusu Simba SC na utendaji wake, huku akiwataka wadau kumuombea kwa Mungu kuelekea siku hiyo atakayofunguka.

“Nitafanya mkutano wiki mbili zijazo na nitaeleza yote kuhusu Simba na utendaji wake, mpira sio ugomvi, ninachowaomba kwa sasa ni mtuombee tu na kumtanguliza Mungu mbele lakini mimi nitafanya mkutano” amesema Mo Dewji

Kwa siku kadhaa za machafuko ndani ya Simba SC, Mo amekua kimya licha ya Wanachama na Mashabiki kutarajia huenda angesema jambo lolote kuhusu kilichokua kikiendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 25, 2021
Kumbe chanzo ni Kocha Nabi!