Kiungo wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Ivan Rakitic ameongeza idadi ya wachezaji majeruhi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Croatia, ambacho kimeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Kosovo na Finland.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Ante Cacic amesema Rakitic ameungana na wachezaji wengine ambao ni majeruhi Luka Modric na Dejan Lovren.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, alifanyiwa upasuaji mdogo mwishoni mwa juma lililopita na hatua hiyo ilipelekea kuukosa mchezo wa ligi ya Hispania ambao ulishuhudia FC Barcelona wakichapwa mabao manne kwa matatu dhidi ya Celta Vigo.

Kikosi cha Croatia kitacheza mchezo wa pili wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Uturuki mwezi uliopita.

Gianni Infantino Apendekeza Timu 48 Kombe La Dunia
Video: Rais wa Congo, Joseph Kabila kuweka jiwe la msingi jengo la TPA leo