Taratibu wa bilionea kijana na mwanachama wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘MO’ za kutaka kuinunua klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa linazidi kunoga baada ya mchana wa leo kukabidhi Shilingi za Kitanzania Milioni 100 kwa Rais wa Simba, Evans Aveva ili kusaidia usajili wa wachezaji.

MO amekabidhi kiasi hicho cha pesa kwenye mkutano na waandishi wa habari ambao Aveva aliongozana na katibu mkuu wa Simba, Patrick Kahemele.

Hata hivyo fedha hizo ni nje ya Ofa ya Bilioni 20 aliyoweka mezani akitaka hisa asilimia 51, huku akitaka mchakato wa kuibadili Simba kwenda kampuni kukamilika si zaidi ya miezi mitatu ijayo.

Jana, uongozi wa Simba ulimuandikia barua kumuomba Mo atoe fedha za usajili kama alivyoahidi kusaidia wakati akitangaza nia yake ya kutaka kununua asilimia 51 za klabu ya Simba.

FIFA Yaipa Heshima Tanzania Kupitia TFF
Mahakama imetangaza tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili Tundu Lissu. Mbunge Nasari aachiwa huru