Kiungo kutoka nchini Misri, Mohamed Naser Elsayed Elneny, amepiga picha kwa mara ya kwanza akiwa amevalia jezi za klabu yake mpya ya Arsenal.
Usajili wa Elneny, ulithibitishwa na meneja wa Arsenal usiku wa kuamkia hii leo, mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Liverpool ambao ulimalizika kwa sare ya mabao matatu kwa matatu.