Beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa mabingwa wa soka Tanzania bara Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema anajivunia kuwa miongoni mwa wachezaji ndani ya kikosi bora cha klabu hiyo.

Tshabalala miongoni mwa nyota wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja ana uhakika wa nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Simba SC licha ya kuwa na ushindani dhidi ya mkali mwenzie, Gadiel Michael, aliyetua kutoka Young Africans mwanzoni mwa msimu huu.

“Nafurahi kuwa hapa na pia kwangu mimi ni heshima kubwa kuchezea Simba, nitazidi kupambana kuhakikisha nakilinda kiwango changu ili nizidi kupata namba chini ya kocha yoyote atakayeinoa Simba,” amesema

Aidha Tshabalala anasema, katika kumbukumbu za maisha yake katika soka, hatasahau kuwa alikuwa sehemu ya wachezaji walioipeleka Simba hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hili jambo halitafutika maishani mwangu, ni historia na itakuwa kumbukumbu yangu maishani”

Nyota huyo amesisitiza mafanikio ambayo klabu yake inayapata yanatokana na umoja uliopo ndani ya timu yao kuanzia viongozi, wachezaji mpaka mashabiki wao.

Mambosasa apiga marufuku mikusanyiko Ufukweni na Bar, Pasaka
Mkuu wa ujasusi awa Waziri mkuu mpya Iraq

Comments

comments