Mabingwa kihistoria barani Afrika timu ya taifa ya Misri wameicharaza Ghana mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi.
Mabao ya Misri katika mchezo huo uliounguruma mjini Alexandria yalifungwa na mshambuliaiji wa klabu ya AS Roma Mohamed Salah pamoja na Abdallah Saied wa klabu ya Al Ahly.
Ushindi huo umeiwezesha Misri kukaa kileleni mwa kundi la tano katika ukanda wa bara la Afrika kwa tofauti ya point mbili wakifuatiwa na Uganda wenye point nne. Misri wamefikisha point sita.
Matokeo ya michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia ukanda wa bara la Afrika:
Libya 0 – 1 Tunisia
Guinea 1 – 2 DR Congo
Cameroon 1 – 1 Zambia
Nigeria 3 – 1 Algeria
Mali 0 – 0 Gabon
Morocco 0 – 0 Ivory Coast
South Africa 2 – 1 Senegal
Cape Verde 0 – 2 Burkina Faso
Uganda 1 – 0 Congo Brazzaville