Mshambuliaji Klabu ya Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka inayotolewa na Shirikisho la wachezji wa kulipwa nchini Uingereza, Proffessional Footballers Association (PFA).

Salah anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Misri na mchezaji wa 7 wa Liverpool kushinda tuzo hiyo.

Tuzo hiyo imekuwa ikiwaniwa na wechezaji wengi na wakubwa katika soka duniani akiwemo, Harry Kane ambaye ni mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, David De Gea, Golikipa wa Manchester United, Kevin De Bryune, David Silva na Leroy Sane ambao ni viungo washumbuliaji wa Manchester City.

Aidha, Leroy Sane amejishindia tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa soka nchini Uingereza. Sane amewashinda Sterling wa Manchester City na Marcus Rashford wa Manchester United.

EXCLUSIVE VIDEO: Tazama Orbit Makaveli akiichambua mistari ya wimbo wake wa “Buku kuwa laki”
Kipchoge aibuka kidedea mbio za London Marathon