Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Misri Mohamed Salah, muda huu anafanyiwa vipimo vya afya mjini Liverpool, kabla ya kukamilisha mpango wa kujiunga na majogoo wa jiji Liverpool FC akitokea AS Roma ya Italia.

Hatua ya upimaji afya kwa mshambuliaji huyo, imeanza mjini Liverpool baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya uhamisho wa Salah, ambao utaigharimu The Reds Euro milioni 39.

Bado haijafahamika kama usajili wa Salah utaweza kuvunja rekodi ya usajili ndani ya klabu ya Liverpool ya Pauni milioni 35, ambayo iliwekwa na mshambuliaji Andy Carroll Januari 2011, baada ya kusajiliwa akitokea Newcastle Utd.

Hali hiyo itategemea na thamani ya pesa kwa siku ya leo, ambapo muda mchache uliopita Euro milioni 39 ilikua sawa na Pauni milioni 34.3.

?Live: Ziara ya Rais Magufuli Mkoani Pwani leo Juni 22, 2017
Juma Jux ahitimu masomo, Vanessa awakejeli waliodai picha za darasani