Kwa mara ya kwanza nchini, Madaktari bingwa kutotka Taasisi ya mifupa na mishipa ya fahamu (MOI) jana ilifanya upasuaji wa ubongo kwa mtoto wa miaka mitano, ikiwa ni tiba ya kifafa kilichomsumbua kwa miaka minne.

Madaktari hao bingwa kutoka hapa nchini walifanikisha upasuaji huo kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchini Cananda.

Bingwa wa upasuaji wa Ubongo, uti wa mgogo na mishipa ya fahamu (MOI), Dkt. Japhet Ngerageza amesema upasuaji huo umefanywa na wataalamu wa Hospitali ya KCMC na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kukubaliana kumfanyia uchunguzi mtoto huyo na kuona inafaa kupasuliwa badala ya kutumia dawa ambazo hazikufanikiwa kumtibu.

Majaliwa aitahadharisha jamii madhara ya ulaji usiofaa

Amesema mtoto huyo amekuwa akipoteza fahamu kwa kuanguka na kupatwa na degedege na ametumia dawa kwa muda mrefu ambazo zimeshindwa kumtibu.

” Upasuaji huo umegharimu sh.200, 000 na kuokoa fedha za matibabu nje ya nchi zilizokuwa zinafikia dola za Marekani 11,000 hadi 15,000, umefanyika kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya kongamano la sita la kufanya uchunguzi na tiba ambalo linahusisha wataalamu wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu” amesema Dkt. Japhet.

Wizara yataka ushirikiano kupandisha hadhi ya chai

ameongeza kuwa ” Kifafa ni ugonjwa ambao unaweza kumkuta mtu yeyote ambaye katika ubongo wake hakuna ‘organisation’ na kusababisha mtu kupoteza fahamu.

Aidha amebainisha  kuwa upasuaji huo umefanikiwa baada ya kuwepo kwa vifaa vya MRI, CT scan, na darubini ya kisasa ambayo imenunuliwa kwa Tsh. Bilioni moja ambayo inarahisisha kuona tatizo kwenye ubongo hata kama ni damu imeganda kwa kiwango kidogo kisichoonekana kwa urahisi.

Mahakama yaamuru Wabunge wa Chadema wenye kesi ya uchochezi wakamatwe
Majaliwa aitahadharisha jamii madhara ya ulaji usiofaa