Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) imekanusha taarifa za kuwa madereva wa pikipiki wakifikishwa hospitalini hapo kwa ajali hukatwa baraka VIUNGO vilivyoumia ikiwemo miguu na mikono.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa bajeti wa taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa lengo la wataalam wa afya na tasnia yao inawataka kulinda kiungo cha muathirika wa ajali kabla ya kufikiria kukikata hivyo sio rahis kuamua kukata kila mgonjwa anaefika hapo bila kuangalia upande wa matibabu na kumpa mgonjwa masaa 12 ya uangalizi.

“Taasisi ya MOI ina jukumu la kutoa tiba za kibingwa kwa magonjwa ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, kufundisha na kuongeza wataalamu wa fani hizi nchini pamoja na kufanya tafiti za magonjwa hayo ili kuboresha tiba, hivyo tunatakliwa kumpa mgonjwa masaa 12 ya kuangalia kama kile kiungo hakitaleta madhara zaidi tunampa tiba ya aina nyingine,” amesema Dkt. Boniface.

Pamoja na hayo Dkt. Boniface amesema kuwa huduma mpya zilizoanzishwa MOI katika kipindi hiki ni huduma ya kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia tundu la pua ambapo wagonjwa 19 wameshafanyiwa upasuaji.

“Gharama za upasuaji huo hapa nchini ni Shilingi milioni 8 na nje ya nchi ni Shilingi milioni 40 hivyo Taasisi imeokoa zaidi ya Shilingi milioni 608,000,000 ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa hao nje ya nchi,” amesema.

Jumla ya wagonjwa 186 wamehudumiwa katika maabara ya upasuaji wa ubongo ambapo gharama za huduma hii hapa nchini ni kati ya Shilingi milioni 5-10 na nje ya nchi ni Shilingi milioni 30 mpaka 60, hivyo Taasisi imeokoa kati ya Shilingi bilioni 5.6 hadi Shilingi bilioni 11.2 ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa hao nje ya nchi.

Huduma hizi mpya, zimeiwezesha taasisi kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa nje ya nchi ambapo kwa sasa kwa magonjwa ya Neurosurgeries kwa 96% tunafanya hapa pamoja na 98% ya upasuaji wa mifupa tunafanya hapa nchini.

Katika kipindi hiki, taasisi iliingia mkataba wa ushirikiano na Chama cha madaktari cha nchini China (CMA) na Hospitali ya Tian Tan ya Beijing China Peking – Katika kuendeleza fani ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 29, 2022
Simba SC yaitosa Azam FC Misri