Mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi, amepinga amri ya Serikali ya Rais Joseph Kabila ya kumpiga marufuku kurudi kwake nchini DRC kutoka uhamishoni Afrika Kusini, kwakuwa ni kinyume cha haki za binadamu.

Gavana huyo wa zamani wa Jimbo la Katanga alipanga kurudi nchini mwake akipitia mjini Lubumbashi, ili kuchukua fomu ya kuwania katika uchaguzi wa urais, lakini hajapewa ruhusa ya ndege yake kutua katika ardhi ya DRC.

Aidha, vyombo vya habari nchini DRC vimeripoti kuwa, Moise Katumbi na washirika wake wanaonekana kupuuzia marufuku ya serikali hiyo, lakini ndege yake binafsi haijapewa ruhusa ya kutua.

Katika barua yake, Meya wa Jiji la Lubumbashi, Ghislain Robert Lubaba Buluma, amesema kuwa ndege ya Moise Katumbi imekataliwa kutua au kupaa katika anga ya DRC.

“Moise Katumbi anakabiliwa na mashitaka ya kuajiri askari mamluki kwa lengo la kuangusha utawala wa Rais Joseph Kabila,” vyanzo kadhaa vya serikali vimeeleza.

Hata hivyo, hatua hiyo imewashangaza wanasheria wa mwanasiasa huyo, ambao wamesema kesi hiyo ilikuwa ikisubiriwa kusikilizwa baada ya kukata rufaa.

 

Luiz Lula Da Silva kugombea tena Urais Brazili
Kangi Lugola aitafutia wateja mahakama ya mafisadi