Kiongozi wa upinzani nchini Congo DR, Moise Katumbi ameahidi kurudi nchini humo mwezi Juni,kuendeleza mpango wake wa kuwania kiti cha urais na kuchukua nafasi ya rais wa sasa, Joseph Kabila katika uchaguzi ulio pangwa kufanyika mwezi disemba mwaka huu.

Katumbi aliondoka Congo DR, Mei 2016 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu nje ya nchi hiyo huku akiwa anashutumiwa kumiliki jeshi binafsi.

“siogopi kurejea Congo’’ Katumbi amewambia waandishi wa habari Jijini Johannesburg,nchini Afrika kusini.

Aidha, Mwanasiasa huyo ambaye pia ni mmiliki wa klabu yaTP Mazembe, anaishi uhamishoni kufuatia kesi zinazomkabili nchini Congo DR ambapo wanasheria wake wanasema madai yanayo mkabili Katumbi yanatokana na shinikizo la kisiasa.

Hata hivyo, hali ya kisiasa nchini DRC imekuwa ikitishia wananchi mbapo ukomo wa utawala wa raisi Kabila umeisha tangu disemba 20, 2016 na uchaguzi umepangwa kufanyika disemba 23, 2018.

Al Ahly yatangazwa bingwa wa Misri kabla ya ligi kumalizika
Cameroon yatangaza nafasi ya kocha mkuu

Comments

comments