Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika ufunguzi wa mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa COP 26 unaojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katika hotuba yake ya ufunguzi alipokaribishwa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ambae ni mwenyekiti wa mkutano huo, Rais Samia amesema Tanzania ni moja ya nchi zinazojitahidi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ingawa changamoto ni fedha.

Rais Samia ameziomba nchi zilizoendelea kuendelea kutoa misaada ya Kifedha kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zina uchumi wa chini ili kuendeleza mipango mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Ufunguzi wa COP 26, huko Glasgow Scotland.

Hii leo Rais Samia anatarajiwa kuhutubia katika mkutano huo.

Shahidi wa Tano akitoa ushahidi kesi ya kina Mbowe
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 2, 2021