Mshambuliaji wa klabu ya Young Africans David Molinga “Falcao” amesema amepokea ofa mbali mbali kutoka kwenye klabu za mataifa tofauti kuelekea msimu ujao wa ligi kuu.

Mshambuliaji ambaye tayari ameshaifungia Young Africans mabao manane msimu huu 2019/20, mkataba wake unafikia tamati mwezi August, huku tetesi zikieleza huenda asisaini mkataba mpya, kufuatia jina lake kuwa sehemu ya wasiohitajika kwenye mipango ya benchi la ufundi la klabu hiyo kwa msimu ujao.

Milinga ambaye kwa sasa yupo nyumbani kwao DR Congo, kufuatia kusimama kwa ligi kuu ya soka Tanzania bara kupisha janga la maambukizi ya virusi vya Corona, amesema moja ya ofa alizopazipa inatolea nchini Morocco.

“Nimepokea ofa kutoka taifa la Moroco,  na wamehitaji kufahamu kutoka kwangu kuhsunmustakabali wa kuendelea kuitumikia Young Africans kuelekea msimu ujao, huku wakinisisitiza niende kufanya nao mazoezi kwa muda wa siku kumi na maongezi ya mkataba yaanze baina yangu na wao.”

“Pia kuna timu tatu nimepokea ofa ya kujiunga nao, lakini nimewaambia wasubiri mpaka mkataba wangu utakapoisha ndani ya klabu yangu.”

“Kwa sasa nawasikiliza viongozi wa Young Africans, kama wakiniambia hawanihitaji basi nitachagua ofa moja kati ya hizo na kujiunga.” Alisema Molinga.

Molinga alisajiliwa na Young Africans mwanzoni mwa msimu huu, akichukua nafasi ya mcongo mwenzake Heritier Makambo aliyetimkia Horoya FC ya Guinea mwishoni mwa msimu uliopita.

Makonda: ''kaka yangu kigwangalla achana na mitandao''
Kituo cha magonjwa ya mlipuko kujengwa ndani ya miezi mitatu Tanzania