Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC) Simba SC Benard Morrison, amefuatilia kesi iliyofunguliwa dhidi yake na uongozi wa Young Africans kwenye mahakama ya usuluhisi katika michezo *CAS*.

Morrison amesikiliza kesi hiyo akiwa jijini Dar ea salaam sanjari na wawakilishi wake kisheria.

Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa kwa mara ya kwanza tangu ilipofunguliwa, imeendeshwa na jaji  Patrick Stewart raia  Uingereza kwa njia ya mtandao.

Young Africans walifungua Mashtaka ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhushi ‘CAS’ dhidi ya hukumu ya Morrison iliyotangazwa mwanzoni mwa msimu wa 2020/21 na kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Kamati hiyo ya TFF ilijiridhisha mkataba uliokuwa unadaiwa upo kisheria baina ya pande hizo una mapungufu, hivyo ilimuweka huru kiungo huyo kutoka Ghana na siku chache alisajiliwa Simba SC.

Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili, mahakama hiyo kupitia kwa jaji Patrick Stewart imesema itatoa hukumu tarehe 24/08/2021.

Kesi ya vigogo wa Simba Agosti 17
Mashabiki, Wanachama watulizwa Young Africans