Inaelezwa kuwa Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umewachukulia hatua za kinidhamu wachezaji Bernard Morrison na Stephanie Aziz Ki, baada ya kurejea nchini.

Wachezaji hao walichelewa kurudi kambini kujiunga na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Mzunguuko wa 20 dhidi ya Ihefu FC, uliopigwa Jumatatu (Januari 16), Uwanja wa Mkapa.

Taarifa kutoka Young Africans zinaeleza kuwa, wachezaji hao tayari wameshajiunga na wenzao kambini, lakini kwa masharti ya kukatwa sehemu ya fedha ya mishahara yao.

Taarifa hiyo imongeza kuwa, Uongozi umefikia maamuzi ya kumkata kila mmoja Shilingi 100,000 kwa Kila siku walizochelewa kufika kambini.

Hata hivyo haijaelezwa kwa kina sababu zilizowachelewa wachezajai hao wa kimataifa kurejea kwa wakati kambini, huku Kocha Nabi akisisitiza kuwa hatavumilia utovu wa nidhamu kwa baadhi wachezaji wake kujiona mastaa kuliko timu.

Wakati huo huo Beki na Kiungo kutoka DR Congo Yannick Bangala ambaye alikuwa sehemu ya wachezaji waliochelewa kufika kambini, amesamehewa na Uongozi kufuatia kutoa sababu zenye mashiko.

Tanzania, Kenya kufanya biashara ya Umeme
Uviko-19: Wizara ya Afya kuzindua dozi ya nyongeza