Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Simba SC lwa mwezi Septemba, akiwashinda Viungo Clatous Chotta Chama (Zambia) na Muzamiru Yassin (Tanzania).

Mapema leo Jumatatu (Oktoba 03), Simba SC imemtangaza Mshambuliaji huyo kupitia kurasa za Mitandao ya Kijamii baada ya kukamilika kwa zaoezi la kupiga kura kupitia Tovuti ya Klabu hiyo.

“Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Septemba inakwenda kwa Moses Phiri. Hongera Phiri 👏 #NguvuMoja” imeeleza taarifa ya Simba SC

Hadi sasa Phiri ndio kinara wa upachikaji mabao katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akifunga mabao manne kwenye michezo mitano aliyocheza, huku akiifungia Simba SC mabao matatu kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mayele: Sitarudia makosa ya msimu uliopita
UN yataka uchunguzi vifo 174 Uwanja wa Mpira