Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake kufuatia vifo 41 na majeruhi 18 vilivyosababishwa na moto kwenye Kanisa la Madhehebu ya Wakristo wa Kikoptiki nchini Misri.

Taarifa ya Msemaji wa Umoja wa Mataifa, iliyotolewa leo jijini New York nchini Marekani imemnukuu Katibu Mkuu, akituma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na Serikali ya Misri huku akiwaombea majeruhi nafuu ya haraka.

Moto huo, uliitokea Agoeti 14, 2022 wakati ibada ikiendelea kwenye kanisa hilo la Abu Sifin mjini Giza nchini Misri, ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari zaidi ya waumini 40 wamefariki na mamia wamejeruhiwa, wakiwemo watoto.

Inaarifiwa kuwa, moto huo uliosababishwa na umeme alianza wakati waumini takribani 5,000 wakiwa kwenye ibada kwenye kanisa hilo lenye ghorofa, na tafrani ilizidi pale ambapo moto huo uliwaka zaidi kwenye eneo la mlango na kuzuia watu kutoka kwa urahisi.

Idara ya zimamoto, iliweze kuzima moto huo lakini hadi sasa chanzo chake halisi hakijaweza kudhihirika.

Kenya: IEBC yabadili kauli 'Ruto hakuongezewa kura'
Republican wamtetea Trump mbele ya vyombo vya Habari