Moto mkubwa uliozuka katika mji wa Pedrogao Grande nchini Ureno umesababisha vifo vya watu 25 na wengine 20 kujeruhiwa vibaya katika mji huo wakiwemo askali wa jeshi la zima moto la nchi hiyo.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Serikali ya Ureno kwa waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Antonio Costa imesema kuwa, janga hilo la moto ni baya zaidi ambalo halijawahi kushuhudiwa siku za hivi karibuni, na kuongeza kuwa haijabainika chanzo cha moto huo ni kitu gani.

Hata hivyo katika kukabiliana na janga hilo la moto, Hispania imetuma ndege mbili ili kuweza kusaidia kuzima moto huo ambao unazidi kusambaa kwa kasi kusini mwa nchi hiyo.

 

 

 

 

Video: Sumaye, Warioba wakoleza moto makinikia ya Acacia, Hakuna kama JPM Afrika
Singida United yapania kufanya makubwa VPL