Waendesha mashtaka wamedai wa kesi ya Mwanaume alieshikiliwa kwa kosa la kuhusika na ulipukaji wa moto wa Bunge la Afrika Kusini wamesema mwanaume huyo alipatikana kwenye eneo hilo akiwa na vilipuzi.

Zandile Christmas Mafe, 49, alifikishwa katika mahakama ya jiji kwa mashtaka chini ya Sheria ya Vilipuzi, pamoja na uchomaji moto, wizi na uvunjaji wa nyumba.

Hata hivyo wakili wake amesema hana hatia katika mashtaka yote ingawa Mafe ndiye mtu pekee aliyekamatwa kuhusiana na moto huo kwa sababu alikutwa na watu wa zima moto ndani ya eneo la tukio wakati wakianza kuzima moto huo.

Mafe alionekana mnyonge na ameduwaa mahakamani, na alipofika kizimbani akiwa amevalia kaptula na shati, alitoa barakoa yake na kuzunguka huku kamera zikimuangazia, anaripoti mwandishi wa BBC kutoka Cape Town.

Kesi hiyo iliahirishwa kwa siku saba ili polisi kuendelea na uchunguzi wao.

Moto huo ulizuka kwa mara ya kwanza Jumapili, na kuharibu kabisa Bunge la Kitaifa, au chumba cha chini cha bunge na siku ya Jumatatu uliripuka tena kwa ukubwa kutokana na upepo uliokuwa ukivuma jijini Cape Town.

Maafisa wa zima moto wanasema wamefanikiwa kuudhibiti moto huo uliozuka siku ya Jumatatu, ingawa hakuna aliyejeruhiwa na moto huo, lakini umeacha taifa na mshangao.

Rais Samia amuwashia moto ‘Ndugai’, asema ana stress za 2025
Dkt. Nchemba ashusha 'nondo' za deni la Taifa, mkopo