Gereza kuu la mji mkuu wa kisiasa wa Burundi, Gitega, limeshika moto usiku wa kuamkia Jumanne na wafungwa wengi wanahofiwa kufariki katika tukio hilo.

Mamlaka nchini Burundi bado haijatoa maelezo kuhusu tukio hili la moto ikiwa picha zilizosambazwa mtandaoni zinaonesha maiti zilizochomwa moto za wale wanaodhaniwa kuwa wafungwa.

Mwandishi wa habari wa shirika binafsi la vyombo vya habari ambaye yuko nje ya gereza hilo anasema zimamoto waliingia ndani ya gereza hilo, lakini sehemu kubwa ya gereza hilo tayari lilikuwa limeteketea.

“Wauguzi wengi wa hospitali ya Gitega walihamasishwa na tuliwaona wakiingia gerezani kusaidia”,

Mfungwa mmoja ambaye alinusurika amesema kuwa moto huo ulizuka mwendo wa saa nne asubuhi katika vyumba vya kulala wafungwa huku wengi wao wakiwa wamelala.

Mwishoni mwa Agosti, moto wa umeme uliteketeza sehemu ya gereza la Gitega, lakini hakuna hasara ya kibinadamu iliyorekodiwa.

Mpaka sasa Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika kwa sasa

Aubameyang kuondoka Arsenal
Lwanga aiwinda Young Africans Dar es salaam