Wafungwa 41 wemefariki dunia na wengine wanane wamejeruhiwa baada ya moto kuzuka katika jengo la gereza karibu na jiji la Jakarta, Indonesian.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo limetokea jana, Septemba 8, 2021 katika jengo linalofahamika kama Block C, kwenye Gereza la Tangerang katika Jimbo la Banten.

Msemaji wa jeshi la Polisi wa Jiji la Jakarta, Yusri Yunus amesema moto huo ulizuka majira ya asubuhi, lakini vikosi vya zima moto vilifanikiwa kuuzima na kuzuia usisambae kwenye majengo mengine ndani ya gereza hilo.

Amesema uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea ingawa taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda ilitokana na hitilafu ya umeme.

Jengo hilo lililoshika moto lilikuwa maalum kwa ajili ya wafungwa wanaoshikiliwa kwa makosa yanayohusu madawa ya kulevya.

Zaidi ya wafungwa 122 walikuwa ndani ya jengo hilo, kwa mujibu wa Yunus. Msemaji huyo wa jeshi la polisi katika jiji la Jakarta amesema jengo hilo lilikuwa na idadi kubwa zaidi ya wafungwa kuliko uwezo wake.

Waziri Bashungwa aiagiza COSOTA kuandaa mpango kazi mkakati wa makusanyo ya mirabaha
Waitara atoa maagizo kwa TANROADS