Moto umezuka leo Septemba 29, 2021 katika shule ya Sekondari Nyehunge iliyoko katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa moto huo umeunguza darasa pamoja na bweni moja katika shule hiyo

Aidha Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo moto huo umeunguza sehemu ya bweni na chumba kimoja cha darasa pamoja na mali za wanafunzi wa kidato cha tano na sita zilizokuwemo bwenini na darasani.

Hata hivyo hakuna madhara ya vifo ama majeruhi kwa wanafunzi, walimu au mtu yeyote ambayo yameripotiwa kutokana na moto huo. Tayari wanafunzi wamewahi kuokoa mali zao na kuziweka sehemu salama ili zizidhurike na moto huo.

Tayari Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kimeshafika eneo la tukio. Taarifa Zaidi tutakuletea hapa hapa.

RC Makalla atangaza Dar Sunset Carnival Coco Beach
KMC FC yatepeta ugenini