Inakadiriwa kuwa, jumla ya watu 13 wamepoteza maisha baada ya kuzuka kwa moto mkubwa uliosababisha kuporomoka kwa dari ya klabu moja ya usiku katika mji wa Kostroma uliopo nchini Urusi.

Taarifa za mamlaka za Serikali na vyombo vya usalama katika eneo hilo zimeeleza kuwa moto huo ulisambaa kwa kasi, katika eneo la takriban mita za mraba 3,500 ndani ya jengo hilo.

Klabu ya usiku ya Poligon nchini Urusi iliyoteketea baada ya paa kushika moto. picha ya Kent Online.

Taarifa hiyo imezidi kueleza kuwa, paa la klabu hiyo ya Poligon, ambayo imekuwa maarufu kwa miongo kadhaa, nalo limeporomoka huku Televisheni ya taifa ya Urusi ikiripoti kuwa watu 250 waliokolewa.

Hata hivyo, chanzo cha moto bado hakijawa wazi lakini vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa fataki iliyofyatuliwa ndani ya jengo hilo, huenda ikawa sababu, na hakuna taarifa rasmi ya chanzo cha tukio hilo.

Marubani 'wapaki ndege' kushinikiza maslahi mazuri
Mafunzo ya dini kuondosha ukosefu wa maadili