Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ Patrice Motsepe, ameweka wazi kuwa mipango yao kwa sasa ni kuhakikisha Soka la Afrika inakuwa na ushindani sawa na Mabara mengine.

Akiongea katika mkutano mkuu wa Shirikisho hilo ambao unafanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha, amesema soka la Afrika lazima likue na ushindani mkubwa kama ilivyo kwa wengine ambapo kama uongozi lazima watalipambania.

Mkutano huo unahusisha wajumbe 156 kutoka nchi 52 wanachama CAF kati ya nchi 154 huku Kenya na Zimbabwe hazijashiriki mkutano huo kutokana na kufungiwa na FIFA.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na zaidi wa watu 400 kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa FIFA, Gianni Infantino, Rais wa Soka Qatar “QFA”, Sheikh Ahmad Thani,waziri mkuu Kassim Majaliwa wengine wengine.

Waziri Mkuu: Mkutano Mkuu CAF utafungua njia kimataifa
Ngilu ailalamikia IEBC kwa kuchapisha jina lake