Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Tunisia Mouez Hassen hatokua sehemu ya kikosi cha timu hiyo, kitakachocheza michezo miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya fainali za kombe la dunia  dhidi ya Panama na Ubelgiji.

Mouez atakua shuhuda wa michezo hiyo baada ya kubainika hatoweza kucheza tena katika kipindi hiki, kufuatia jeraha la bega alilolipata dakika ya 16, wakati wa mchezo dhidi ya England, uliomalizika kwa Tunisia kukubali kufungwa mabao mawili kwa moja.

Mouez anaeitumikia klabu ya Chateauroux inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ufaransa, alilazimika kutoka nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na mlinda mlango chaguo la pili Farouk Ben Mustapha.

Uongozi wa klabu ya Chateauroux umetoa taarifa za kumsafirisha mlinda mlango huyo hadi Ufaransa, kwa matibabu zaidi.

Mouez mzaliwa na Ufaransa, aliamua kuitumikia timu ya taifa ya Tunisia mapema mwaka huu.

Moeuz alichukua maamuzi hayo baada ya kuona ana nafasi finyu ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Sugu: Mimi sio kama Roma, Nitaiburuza Basata mahakamani
Pellegrini amrudisha Lukasz Fabianski ligi kuu