Meneja mpya wa klabu ya Man Utd, Jose Mourinho amedhamiria kulipa kisasi dhidi ya mwajiri wake wa zamani Chelsea, kwa kufanya kila linalowezekana katika msimu ujao wa ligi ya nchini Engalnd.

Mourinho alithibitishwa jana jioni kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ya Old Trafford baada ya kukamilisha dili la kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 53, amejizatiti kulipiza kisasi dhidi ya Chelsea ili kuuonyesha umma kwamba, uongozi wa The Blues ulifanya makossa kumfuta kazi mwishoni mwa mwaka 2015.

Rafiki wa karibu wa Mourinho, amefanya mahojiano na gazeti la The Sun la nchini England, na kueleza mpango wa meneja huyo ambao ana uhakika wa kuukamilisha kwa vitendo.

“Lengo kubwa la Mourinho ni kuipa ubingwa Man Utd kwa njia za kiushindani na hapa hamaanishi kama atakuwa na lengo la kuifunga Chelsea pekee yake, bali anataka kudhihirisha bado ana ubora wa kufanya kazi yake ipasavyo.

“Jose daima anaipenda Chelsea na amekua akifuatilia kwa ukaribu kinachofanyika huko magharibi mwa jijini Lonndon, lakini kwa hatua ya kukabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha Man utd, hana budi kufanya kazi yake ipasavyo na kuweka pembeni urafiki uliojengeka baina yake na The Blues.

“Ni kweli kwa siku nyingi Jose alihitaji kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Man Utd baada ya kuwa pembeni na shughuli za umeneja mwishoni mwa mwaka jana, na sasa dhamira yake ni moja tu, ya kuendelea kuthibitisha uwezo wake wa kufundisha soka.” Alisema rafiki huyo wa karibu wa Mourinho ambaye hakutaka jina lake kutajwa hadharani.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Man Utd umetangaza kutenga kiasi cha Pauni Milioni 200 kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya, ambao watapendekezwa na Jose Mourinho.

Chelsea Kumrejesha Romelu Lukaku Stamford Bridge
Cannavaro Asafiri Na Taifa Starts Hadi Nairobi - Kenya