Meneja wa klabu bingwa nchini England, Chelsea Jose Mourinho ameendelea kulipa nafasi suala la mshambuliaji wake kutoka nchini Hispania Diego Costa anaetumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na chama cha soka FA, katika mikutano yake na waandinshi wa habari.

Mourinho alizungumza suala la mshambuliaji huyo ambaye aliadhibiwa kutokana na kitendo cha kumpiga kwa makusudi beki wa klabu ya Arsenal,  Laurent Koscielny wakati wa mchezo wa ligi uliochezwa Septemba 19, katika mkutano wake uliokua unazungumzia mchezo wa hii leo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo The Blues watapambana na FC Porto huko nchini Ureno.

Mourinho, amesema anaamini adhabu ya mshambuliaji huyo, ilitolewa kwa maslahi ya watu wachache baada ya kulalamika kwa kuona Costa alipaswa kuadhibiwa lakini kwake haamini kama ilistahili.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, ameendelea kumtetea mchezaji wake kwa kuamini hakufanya kosa lolote wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Arsenal, na ataendelea kujivunia kuwa na Diego Costa katika kikosi chake.

Hata hivyo Costa hii leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea baada ya kukosa mchezo wa ligi ya nchini England mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Chelsea walilazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Newcastle Utd.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, hii leo atacheza mchezo dhidi ya FC Porto kutokana wigo wa adhabu yake kutokuhusika kwenye michuano ya barani Ulaya ambayo ipo chini shirikisho la soka barani humo UEFA.

Blatter, Platini Watangaza Misimamo Yao
Mtoto Wa Paul Walker Afungua Mashtaka Kuhusu Gari Lililochukua Uhai Wa Baba Yake