Mtarajiwa wa Man Utd, Jose Mourinho ameonekana katika viunga vya magharibi mwa jijini London, akisimamia zoezi la kufungasha vifaa ambavyo vipo tayari kwa kusafirishwa nje ya mji.

Mourinho ameokeana katika usimamizi huo, ikiwa ni siku moja baada ya aliyekua meneja wa Man Utd, Louis Van Gaal kutimuliwa kazi na uongozi wa klabu hiyo kwa kigezo cha kushindwa kuipeleka The Red Devils, kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Kitendo hicho kimezungumzwa kama kuiva kwa taratibu za kutangazwa kwa Mourinho kama meneja mpya wa Man Utd, baada ya kubainika alikua akifungasha kila kilicho chake huko magharibi mwa jijini London, tayari kwa safari ya kuelekea mjini Manchester.

Mourinho, mwenye umri wa miaka 53, anapewa nafasi kubwa ya kutangazwa kuwa meneja wa Man Utd, ndani ya juma hili, kwa kuaminiwa ndiye chaguo sahihi la kurejesha heshima Old Trafford.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba Mourinho, huenda akasainishwa mkataba wa miaka mitatu, ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni milioni 60 kwa mwaka.

Pep Guardiola Kuanza Na Ilkay Gundogan
Maalim Seif Mikononi mwa Polisi

Comments

comments