Meneja wa Man Utd Jose Mourinho, ameitega klabu ya Southampton kwa kutaka kufanya biashara ya kumpeleka beki wake kutoka nchini Argentina Marcos Rojo St Mary’s Stadium kwa kumlenga beki wa The Saint, Jose Fonte.

Mourinho amedhamiria kufanya hivyo kwa kuamini Fonte ataweza kwenda sambamba na kasi yake, tofauti na Rojo ambaye ameonyesha kuwa katika kiwango cha kawaida tangu aliposajiliwa na meneja aliyemtamnguli Louis Van Gaal.

Fonte, mwenye umri wa miaka 32 amekua akifuatiliwa kwa ukaribu na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger na inahisiwa huenda akawa katika mipango ya mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, kutokana na tatizo la safu ya ulinzi linalomkabili kwa sasa.

Leicester City v Manchester United - The FA Community ShieldMarcos Rojo akiwania mpira dhidi ya kiungo wa Leicester City Riyad Mahrez wakati wa mchezo wa ngao ya jamii.

Hata hivyo Mourinho ameonyesha kuwa tayari kupambana na Wenger katika harakati za kumsajili beki huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ureno ambacho kilitwaa ubingwa wa Euro 2016 katika ardhi ya Ufaransa miezi miwili iliyopita.

Fonte, ana uzoefu wa kutosha katika soka la nchini England baada ya kuitumikia Southampton katika michezo 250 ndani ya miaka sita, na alikuwa katika kikosi kichopambana na Watford mwishoni mwa juma lililopita na kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Pamoja na mpango huo wa Mourinho wa kutaka biashara ya kubadilisha wachezaji, meneja wa Southampton Claude Puel amesisitiza kutokua tayari kuona Fonte anaondoka.

Yametimia - Jonathan Calleri Akabidhiwa Nyundo Za London
Chelsea Yajaribu Tena Kwa Kalidou Koulibaly