Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, amejiiingiza kikaangoni kwa mara nyingine tena, kufuatia kauli aliyoitoa mara baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev.

Mourinho amemchambua muamuzi aliyepewa jukumu la kuchezesha mchezo huo uliounguruma mjini Kiev usiku wa kuamkia hii leo, Damir Skomina kwa kusema hakuitendea haki timu yake kutokana na mapungufu makubwa ambayo aliyaonyesha hadharani.

Mourinho, ametoa kauli hiyo huku akiwa bado ana kumbu kumbu ya kufungiwa mchezo mmoja wa ligi ya nchini England pamoja na kutozwa faini ya paund elfu 50, kutokana na maneno makali aliyoyatoa mbele ya waandishi wa habari, dhidi ya muamuzi aliyechezesha mchezo ulioshuhudia Soputhampton waliochomoza na ushidni wa mabao matatu kwa moja kwenye uwanja wa Stamford Bridge mwanzoni mwa mwezi huu.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, amedai kwamba muamuzi Damir Skomina, alishindwa kutoa haki kwa Chelsea kwa kuwanyima penati ya dhahir kufuatia madhambi aliyofanyiwa kiungo wake kutoka nchini Hispania, Cesc Fabregas, katika kipindi cha kwanza.

Mourinho alisema muamuzi huyo kutoka nchini Slovenia, alikua mvivu kwa kushindwa kwenda sambamba na kasi ya mchezo na wakati mwingine alikua anashindwa kufika katika maeneo yaliyokua yakihusisha matukio mazito mazito.

Kufuatia kauli hiyo ya Mourinho, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, linatarajiwa kutoa maamuzi ndani ya saa 48, baada ya kupitia ripoti ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Magufuli Ageukia Kura Za Ushindi Dar
Guardiola: Sina Desturi Ya Kumlaumu Mchezaji