Chama cha soka nchini England FA, kimetoa taarifa za kutomchukulia hatua zozote za kinidhamu meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho kufuatia sakata la aliyekua daktari wa kikosi cha klabu hiyo, Eva Carneiro lililotokea mwanzoni mwa msimu huu.

FA, walikua wakifanya uchunguzi dhidi ya Mourinho, baada ya kuibuka kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia, ambapo meneja huyo kutoka nchini Ureno alidaiwa kuufanya wakati alipokua akimkalipia Eva Carneiro alipoingia uwanjani kwenda kumpa huduma ya kwanza Eden Hazard.

Uchunguzi wa FA umeshindwa kudhihirisha ukweli wa maneno yaliyozungumzwa na Mourinho hivyo wameamua kuiweka pembeni kesi hiyo.

FA, walilazimika kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo baada ya kushawishiwa na vyombo vya habari ambavyo vilijitahidi kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo na vilibaini maneno ya unyanyasaji yaliyozungumzwa na Mourinho kwa kuweka picha za televisheni kwenye mitandao.

Hata hivyo vyombo hivyo vya habari vilikwenda mbali zaidi, kwa kuandika maneno ya unyanyazaji yaliyozungumzwa na Mourinho dhidi ya Eva Carneiro wakati akiingia uwanjani na alipotoka.

Neno kubwa ambalo lilipewa nafasi ya kujadiliwa na kuandikwa na vyombo vya habari vya nchini England, ni lile lililodhihirisha kumtusi Eva Carneiro kwa kuitwa mtoto wa kahaba.

Eva Carneiro, ameshaondoka kwenye klabu ya Chelsea, na amekataa kurudi kazini baada ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa klabu hiyo huku akisistiza kusaka ushauri wa kisheria ili aweze kulifikisha suala lake kwenye vyombo vya sheria kusaka haki dhidi ya Jose Mourinho.

Mbatia Aeleza Njama Za Kutaka Kuuawa Na Kudhoofisha Ukawa
Abiria 900 Waliokwama Na Treni Dar Wapaza Sauti